UKAME WA MABAO WAMUUMIZA KICHWA GIROUD


Mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud amekiri kuwa anaumia kushindwa kufunga mabao akiwa na matajiri hao wa London.

Mfaransa huyo amefunga bao moja tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Arsenal mwezi Januari huku akisaidia mabao matatu katika mechi nane alizocheza mpaka sasa.

Giroud 30, hana uhakika wa kuwemo kwenye kikosi cha Ufaransa kitaka choshiriki kombe la dunia na moja ya sababu iliyomfanya kuondoka Arsenal ili kupata nafasi.

Ingawa ameanza kwa changamoto maisha yake ndani ya Chelsea, Giroud anaamini atafanikiwa zaidi akiwa Stamford Bridge.

“Nina furaha kwa jinsi nilivyoweza kuzoea mazingira ya hapa, pia jinsi nilivyopokelewa na ushirikiano ndani ya uwanja ninaopata kutoka kwa wachezaji wenzangu.

"Natakiwa kufunga mabao mengi zaidi, kwa mujibu wa takwimu nimefunga bao moja na kusaidia mengine matatu tangu nije hapa," alisema Giroud.

No comments

Powered by Blogger.