SAMUEL UMTITI NJIA NYEUPE KWENDA MAN UNITED
Habari
zilizoripotiwa na mtandao wa SPORT nchini Spain zinaeleza kwamba Barcelona
wanajiandaa kuachana na beki wake raia wa Ufaransa Samuel Umtiti.
Umtiti amehusishwa Kwa kiasi kikubwa kuhamia
Manchester United msimu ujao kufuatia makubaliano kuongezwa mshahara ili asaini
mkataba mpya na Barcelona kuyumba kwani mchezaji huyo anataka alipwe kiasi cha
pesa anacholipwa Andreas Iniesta kitu ambacho Barcelona hawakubaliani
nacho.
Paundi milioni 50 ndizo hasa zinazoweza kumtoa
mchezaji huyo Barcelona kabla ya mkataba wake kumalizika na tayari United
wameonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo wakiwa tayari kulipa kiasi cha
mshahara anachotaka.
Umtiti amebakiza miaka mitatu kuitumikia
Barcelona na klabu hiyo ilimpa tu kipaumbele cha kujadiliana nae kuhusu mkataba
mpya.
Wakati huu ambao Barcelona wanajiandaa kumsajili
Antoine Griezman ambaye atalipwa si chini ya Paundi milioni 13 Kwa mwaka,
wanapaswa kupunguza matumizi yao pia na hii inaleta ugumu Kwa Umtiti
kubaki.
Tayari Clement Lenglet kutoka Sevilla ambaye
anapatikana Kwa kiasi cha Paundi milioni 26 tu anatajwa huenda akasajiliwa
kuchukua nafasi ya Umtiti Barcelona.
No comments