SAA CHACHE BAADA YA KUITWA TIMU YA TAIFA, WELBECK ATUPIA 2 ARSENAL IKITINGA ROBO FAINALI

Arsenal 3-1 AC Milan (5-1 agg): Danny Welbeck double and Xhaka score
Mshambuliaji wa kimataifa wa England anayeichezea Arsenal Danny Welbeck jana aliiwezesha Arsenal kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa league akifunga mabao mawili katika ushindi wa bao 3-1 walioupata Arsenal usiku wa jana dhidi ya AC Milan.

Ni saa chache tu zilipita tangu mshambuliaji huyo alipoitwa katika kikosi cha England ambacho kitaivaa Uholanzi na Italia katika mechi mbili za Kirafiki wiki ijayo na kwa kufunga mabao hayo imemuongezea morali kwa ajili ya kujiongezea nafasi ya kuitwa katika kikosi kitakachoshiriki kombe la dunia.

Goli lingine la Arsenal lilifungwa na Granit Xhaka kuifanya timu hiyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa bao 5-1 baada ya ushindi wa bao 2-0 walioupata wiki iliyopita.

Sambamba na Arsenal timu zingine 7 zimetinga hatus hii nazo ni Lazio, Atletico Madrid,Olympic Marseille,Sporting Lisbon, CSKA Moscow, RB Salsburg na RB Leizpig huku Droo ya hatua hiyo ya Robo fainali ikipangwa kufanyika leo mchana mara baada ya droo ya Ligi ya mabingwa barani ulaya 



No comments

Powered by Blogger.