RONALDO AJIWEKEA REKODI NYINGINE URENO
Mchezaji bora wa soka duniani na nahodha wa timu ya
taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo jana alijiwekea rekodi ya kuwa mchezaji wa
kwanza anayeendelea kucheza soka mwenye mabao mengi zaidi katika timu yake ya
Taifa akifunga mabao yaliyoiwezesha Ureno kushinda bao 2-1 dhidi ya Misri.
Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki ulikuwa moja
kati ya michezo mingi iliyopigwa jana katika mwendelezo wa mechi za kimataifa
za kirafiki katika kalenda ya FIFA.
Mpaka dakika ya 90 Ureno walikua nyuma Kwa bao 1-0
dhidi ya Mafarao hao wa Misri goli lililofungwa na Mohamed Salah dakika ya 56
na wengi wakiamini kama mchezo huo ungeisha hivyo ndipo Ronaldo alipofanya yake
90'+2 ⚽ Cristiano
Ronaldo
90'+4 ⚽ Cristiano
Ronaldo
Baada ya kufunga magoli hayo Ronaldo sasa amefikisha
magoli 81 akiwa na timu yake ya Taifa akishika nafasi ya kwanza kati ya
wachezaji waliofunga mabao mengi wanaoendelea kuzichezea timu zao za taifa na
amekuwa mchezaji wa tatu katika orodha ya wachezaji wa muda wote walioweza
kufunga mabao mengi wakiwa na timu zao za Taifa.
![]() |
| Ali Daei (Mchezaji wa zamani wa Iran) |
ORODHA YA WAFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE
- Ali Daei (Mchezaji wa zamani wa Iran) - 109
- Ferenc Puskas (Mchezaji wa zamani wa Hungary) - 84
- Cristiano Ronaldo (Nahodha wa sasa wa Ureno)
- 81
Ronaldo bado Ana nafasi ya kuweza kuwapiku Ali Daei
anayeongoza orodha hiyo pia nafasi iko wazi kuweza kumzidi Puskas
anayeshika nafasi ya pili.
Ikumbukwe...
Tarehe 12 Juni 2004 Cristiano Ronaldo alifunga bao
lake la kwanza akiichezea Ureno na jana
tarehe 23 Machi 2018 amefunga bao la 80 na 81 akiwa na Ureno.



No comments