MAKAMU WA RAIS TFF AFUNGIWA MAISHA KWENYE SOKA.
Michael Wambura ambaye ni Makamu wa Rais wa
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) amekutwa na makosa matatu ya
kimaadili ambayo yalifanyika miaka 14 iliyopita.
Akisoma hukumu hiyo Afisa habari wa shirikisho
la Soka nchini TFF, Cliford Mario Ndimbo kwa niaba ya Kamati ya Maadili ambayo
iko chini ya Mwenyekiti Hamad Mbwezeleni ametaja makosa hayo kuwa ni
1. Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF)
za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha
kanui za Maadili za TFF Toleo la 2013
2. Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo
ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni
kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013
3. Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho
ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa
mwaka 2015).
Kamati ya Maadili ya TFF iliyoketi jana Machi 14
imemfungia Michael Wambura maisha kutojihusisha na soka baada ya kujiridhisha
kuwa ametenda makosa tajwa hapo juu ikumbukwe katika Soka la Tanzania Wambura
Huyu Huyu aliwahi kufungiwa na klabu ya Simba kutokana na kupeleka maswala ya
Soka mahakamani.

No comments