KROOS KUCHUKUA NAFASI YA POGBA MAN UNITED

Gazeti la Metro limeripoti kuwa Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho yupo tayari kumuuza Paul Pogba majira ya joto yajayo na kumnunua kiungo wa Real Madrid, Toni Kroos kuchukua nafasi yake.

United ilivunja rekodi ya usajili mwaka 2016 ya kumrejesha Pogba Old Trafford lakini ujio wake umekuwa tofauti na matarajio ya Mashetani hao.

Pogba ameanza mechi nne katika michezo 11 ya United iliyopita huku akiwekwa benchi katika mchezo wa robo fainali wa  FA dhidi ya Brighton wiki iliyopita.

Sunday Mirror limeripoti kuwa Mourinho anajiandaa kutumia kiasi kikubwa cha pesa dirisha lijalo la usajili huku Kroos akiongoza orodha ya wanaohitajika Old Trafford.

Mjerumani huyo alikaribia kujiunga na United miaka minne iliyopita kabla ya kuamua kwenda Madrid akitokea Bayern Munich.

Kroos amefunga mabao manne na kusaidia mengine saba wakati Pogba amefunga matatu na kusaidia 10 msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.