YANGA YATOA ONYO IRINGA YAICHAKAZA LIPULI
Ushindi huo unaotajwa kuwa wa kwanza kwa Yanga katika uwanja huo ulianza kuonekana dakika ya 19 ya baada ya Pappy Tshishimbi kuukwamisha wavuni mpira uliotemwa na golikipa wa Lipuli, Agaton Mkwando wakati akipangua mpira wa kichwa wa Emmanuel Martin.
Bao hilo lilidumu hadi mapumziko, ambapo kipindi cha pili Yanga waliongeza bao lingine lililofungwa na Pius Buswita dakika ya 55 baada kumalizia mpira uliopigwa Obrey Chirwa.
Kwa ushindi huo, Yanga wamefikisha alama 31 ikiwa nafasi ya pili kufuatia Azam FC kuwa dimbani muda huu kucheza na Ndanda FC katika uwanja wa Azam Complex.
No comments