YANGA YASHINDA LAKINI MAMBO BADO

A imeanza vema michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa bao dhidi ya St Louis ya Shelisheli mchezo uliofanyika kwenye wa taifa.

Hata hivyo Yanga haipaswi kubweteka na ushindi huo kwani mchezo wa marudiano utakaofanyika visiwa vya Shelisheli unatarajia kuwa magumu kwao.

Bao hilo pekee la Yanga lilifungwa na Juma Mahadhi dakika ya 67 muda mfupi baada ya kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajibu ambaye hakuwa na mchezo mzuri leo.

Yanga ilitawala zaidi mchezo huo ikipata kona nyingi kuliko wapinzani wao ambao walikuwa wakijilinda muda mwingi.

St Louis walicheza vizuri dakika 15 za kwanza za kipindi cha pili kwa kufanya mashambulizi kadhaa ambayo hayakuwa na madhara kwa Yanga.

Mchezo wa marudiano utapigwa visiwani humo Februari 20 mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.