YANGA YAENDELEA KUZIPA PRESHA SIMBA,AZAM
Mabingwa watetezi wa ligi kuu timu ya Yanga imeendelea kuzipa presha Azam FC na Simba baada ya kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Njombe Mji jioni ya leo.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuzidiwa pointi nne na Simba huku ikiizidi Azam pointi moja huku miamba hiyo ikikutana yenyewe kesho katika muendelezo wa ligi hiyo.
Njombe Mji waliwamudu vizuri Yanga hasa kipindi cha kwanza kwa kufanya mashambulizi kadhaa langoni lakini mlinda mlango kinda Ramadhan Kabwili alikuwa kikwazo.
Yanga ilipata bao la kwanza kupitia kwa Obrey Chirwa dakika ya 47 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Pius Buswita kutoka upande wa Kulia.
Dakika ya 56, mlinda mlango wa Njombe Mji Rajabu Mbululu alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuudaka mpira aliorudishiwa na beki wake akiwa nje ya eneo lake na kuwafanya Njombe kucheza wakiwa pungufu.
Chirwa alifunga bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 64 kabla ya Emmanuel Martin kufunga la tatu dakika ya 84.
Chirwa alikamilisha ushindi huo kwa kufunga bao la nne likiwa la tatu kwake 'hat trick' dakika ya 88 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Baruhan Yahaya.

No comments