SPORTPESA YAZINDUA KITENGO KIKUBWA CHA HUDUMA KWA WATEJA NCHINI
Kampuni
ya michezo ya kubashiri ya SportPesa leo February 1, imezindua rasmi kitengo
cha huduma kwa wateja ili kuendelea kuboresha huduma zao.
SportPesa
kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Utawala na Udhibiti, Ndugu Tarimba Abbas, imeujulisha
umma kuwa kitengo maalum cha huduma kwa wateja, kilikuwa kikiendesha shughuli zake
nchini Kenya ambapo ndipo yalipo makao makuu ya kampuni hiyo.
“Ili
kuboresha zaidi huduma zetu tumehamishia kitengo chetu cha huduma kwa wateja katika
ofisi zetu za hapa Dar es Salaam ili kuonyesha ni jinsi gani tunawajali na kuwafikiria
wateja wetu kwa kusogeza huduma karibu yao.
“Kutokana
na moja ya changamoto ambazo vijana wanapitia kuwa ni ajira, sisi kama SportPesa
tumeajiri vijana wapatao 84 kwenye kitengo chetu na vijana hawa wamefanyiwa
mafunzo jinsi ya kuwasikiliza na kuwahudumia wateja kwa uzoefu wa hali juu.
“Kama
mnavyojua sisi tutakuwa ni kampuni ya kwanza ya michezo ya kubashiri yenye
huduma kwa wateja wake saa 24 siku 7 za wiki, hii inaonyesha ni namna gani
mteja wetu ni kipaumbele namba moja”, alifafanua Ndugu Abbas.
Wateja
wa SportPesa wanaweza kuendelea kuwasiliana na huduma kwa wateja saa 24 kila
siku kupitia nambari 0764 115588, 0692 115588 na 0685 115588 kwa msaada Zaidi.
Mkurugenzi
huyo aliwaomba watanzania kuendelea kuiunga mkono kampuni hiyo ambayo
imedhamiria kuleta sura mpya kwenye sekta ya michezo nchini sambamba na
kubadilisha maisha ya mtanzania mmoja mmoja kupitia program mbalimbali ikiwa ni
pamoja na promosheni ya siku 100 ya TVS KING DELUXE ambayo inatarajia kufika
tamati siku ya kesho.
SportPesa
ndio mdhamini mkuu wa vilabu vya Simba na Yanga pamoja na Singida United kwa
nchini Tanzania na sasa wako ukingoni mwa promosheni yao ijulikanayo kama
SHINDA NA SPORTPESA ambapo washindi 100 wa bajaji aina za TVS KING wamepatikana
katika promosheni hiyo na kuweza kubadili
maisha yao.
namba hatupati huduma ni matangazo tu mpaka dk zinaisha
ReplyDeleteNamba hazipatikani ,mbona kama utapeli
ReplyDelete