SIMBA YAREJEA KIMATAIFA NA 4G
Vinara wa ligi kuu Soka Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba Leo wamerejea katika anga za kimataifa Kwa kuifunga Gendermerie ya Djibouti Kwa bao 4-0
Mchezo huo wa kombe la Shirikisho barani Afrika ulichezwa jioni hii katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam huku Simba wakionekana kuwa bora zaidi Kwa dakika zote za mchezo huo.
Mpaka Mapumziko Tayari Simba walishakua mbele Kwa bao 3-0 magoli mawili ya Nahodha John Bocco na moja la kiungo Said Ndemla.
Kipindi cha Pili Gendermerie walifanikiwa kupata penati lakini kipa wa Simba Aishi MANULA alifanikiwa kuokoa penati hiyo.
Emmanuel Okwi ambaye Leo alikosa mabao kadhaa ya wazi ndiye aliyefunga bao la 4 dakika za nyongeza za kipindi cha pili Ikiwa ni mpira wa adhabu ndogo na kufanya Simba kuibuka na ushindi huo muhimu nyumbani wakisubiri mechi ya marudiano

No comments