SIMBA KAMA KAWA YAICHAPA TENA RUVU

Wekundu wa Msimbazi Simba wameendelea kutoa dozi baada ya ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Ruvu Shooting katika muendelezo wa ligi kuu ambayo imeanza mzunguko wa pili wikiendi hii.

Katika michezo mitano ya Simba iliyopita imeshinda yote ikifunga mabao 15 bila kuruhusu bao ikionyesha wazi ina safu imara ya ushambuliaji na ulinzi pia.

Mchezo huo ulishuhudiwa nahodha John Bocco akiendelea kung'aa baada ya kufunga mabao mawili wakati kiungo Mzamiru Yassin akitupia moja.

Bocco amefikisha mabao tisa akishika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji wa ligi.

Mshambuliji nyota wa Simba Emmanuel Okwi alishindwa kuendelea na mchezo huo akitolewa dakika ya 45 baada ya kupigwa ngumi na mlinzi Mau Bofu ambaye alionyeshwa kadi nyekundu.

Hii ina maana Simba imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 38 ikiizidi Azam FC iliyo namba mbili kwa pointi tano.

No comments

Powered by Blogger.