OKWI NOMA AIBEBA SIMBA KIMATAIFA, SASA KUWASUBIRI WA MISRI.

Mshambuliaji Mkongwe wa Wekundu wa Msimbazi Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania bara kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika Emmanuel Okwi ameibuka shujaa wa timu yake baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gandermarie ya Djibouti.

Simba iliingia katika Mchezo wa leo ikiwa na faida ya ushindi wa bao 4-0 walioupata Dar es Salaam wiki iliyopita.

Mpaka mapumziko Hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake lakini dakika ya 53 Emmanuel Okwi alifanikiwa kufunga bao Hilo pekee baada ya kukimbia na mpira upande wa kulia na kuwazidi ujanja mabeki wa Gendarmerie na kuukwamisha mpira wavuni kuandika bao pekee katika mchezo huo.

Simba sasa inaingia hatua ya kwanza ambapo itacheza dhidi ya Al Masry ya Misri

No comments

Powered by Blogger.