OKWI MTU MBAYA, GOLI LAKE LAWALIZA AZAM FC UWANJA WA TAIFA

Kinara wa mabao katika ligi kuu Soka Tanzania bara Emmanuel Okwi ameendelea kuonyesha utofauti mkubwa katika kikosi cha Vinara wa ligi kuu Soka Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba akifunga bao pekee Leo dhidi ya Azam FC katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Okwi mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Uganda ambao mashabiki wanapenda kumwita Mhenga alifunga bao pekee dakika ya 36 baada ya kazi nzuri ya Asante Kwasi ambaye alikimbia na mpira na kupiga krosi iliyomkuta mfungaji akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa Azam FC.

Kipindi cha kwanza Simba walionekana kuwa bora kabisa kipindi cha kwanza wakati Azam walikua vizuri sana kipindi cha pili huku kipa wa Azam FC akifanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Emmanuel Okwi

Matokeo ya Leo yanaifanya Simba kufikisha pointi 41 katika nafasi ya kwanza Ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa mchezo wowote inafatiwa na Yanga wenye pointi 34 wakati Azam FC na Singida United zote zina pointi 33.

Katika michezo mingine Leo MTIBWA wakisafiri mpaka Mwadui walikubali kichapo cha bao 3-1 toka kwa Wenyeji Mwadui huku Singida United ikishinda 2-1 ugenini dhidi ya Mbao FC ya Jijini Mwanza.

No comments

Powered by Blogger.