MTIBWA HIYOOOO ROBO FAINALI KOMBE LA FA.

Ndoto za klabu ya Buseresere ya Mjini Geita kutinga hatua ya Robo fainali katika michuano ya Azam Sports Federations Cup maaruufu kama Kombe la FA zimeyeyuka baada ya kukubali kicha bao 3-0 toka kwa Mtibwa Sugar.

Pambano Hilo lilichezwa kwenye uwanja Mkongwe wa Nyamagana jijini Mwanza ambapo mpaka mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.

Kipindi cha Pili Mtibwa Sugar waliamka na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 52 likifungwa Kwa njia ya penati baada ya Michae Aidan kuangushwa eneo la hatari na mwamuzi kuamua iwe penati.

Haruna Chanongo aliongeza  bao la pili Kwa Mtibwa dakika ya 83 kisha Ally Makarani akaandika bao la tatu dakika za nyongeza Kwa shuti Kali nje ya kumi na nane.

Mtibwa Sugar imeungana na Singida United, Azam FC, Njombe Mji na Yanga kucheza hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo ya pili Kwa ukubwa katika ngazi ya klabu ambapo bingwa wake ataiwakilisha nchi katika kombe la Shirikisho barani Afrika.

No comments

Powered by Blogger.