MRITHI WA MWESIGWA TFF KUTANGAZWA MUDA WOWOTE
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema muda si mrefu kutoka sasa Katibu mkuu wa Shirikisho hilo atatangazwa baada ya taratibu zote kufuatwa.
Nafasi hiyo inakaliwa na Mwesigwa Celestine ambaye anashikiliwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi sambamba na Rais wa zamani wa Shirikisho hilo Jamal Malinzi.
Karia amesema hayo katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha luninga cha Clouds TV kuwa ndani ya siku chache zijazo atatangazwa katibu mkuu atakaye chukua nafasi ya Mwesigwa.
Wilfred Kidao anakaimu nafasi hiyo kwa miezi kadhaa sasa huku Rais Karia akisema ameridhishwa na utendaji wake wa kazi.
"Suala la katibu mkuu litakamilika muda mfupi ujao, Kidao amekaimu kwa muda sasa lakini haiwezi kuwa hivyo kwa kipindi kirefu kuna taratibu tunamalizia kisha tutamtangaza," alisema Rais Karia.
Hata hivyo Kidao anapewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo moja kwa moja.

No comments