MASKINI CHELSEA YAPIGWA TENA KATIKA EPL SAFARI HII NI 4G

Watford 4-1 Chelsea: Deulofeu and Janmaat net late goals
Hali imeendelea kuwa tete kwa kikosi cha mabingwa wa ligi kuu ya England Chelsea baada ya jana kufungwa tena kwa bao 4-1 dhidi ya Watford katika mchezo wa ligi kuu ya England uliochezwa jana Usiku katika dimba la Vicarage Road.

Troy Deeney alitangulia kuipatia Watford bao la kwanza kwa penati baada ya kipa wa Chelsea kumwangusha Gerard Deulofeu kisha Eden Hazard akaisawazishia Chelsea lakini haikutosha kwani Daryl Janmaat, Roberto Pereyra na Gerard Deulofeu walifunga bao moja kila mmoja kukamilisha kipigo hicho cha bao 4-1.

Hii inakuja siku chache baada ya Chelsea kukubali kichapo cha bao 3-0 katika mechi iliyopita dhidi ya AFC Bournemouth katika uwanja wa Stamford Bridge.

No comments

Powered by Blogger.