COUTINHO AFUNGUA UKURASA WA MABAO, BARCELONA IKITINGA FAINALI COPA DEL REY
Countinho alianzia benchi katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Mestalla ukiwa ni mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya kombe la Mfalme maarufu kama Copa del Rey huku mchezo wa awali uliipa Barcelona faida baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Phillipe Countinho aliingia kipindi cha pili kilipoanza akichukua nafasi ya Andre Gomes na dakika tatu baadae akaweza kuifungia timu yake bao la kwanza baada ya kipindi cha kwanza kumalizika ikiwa ni bila bila. Bao la pili la barcelona lilifungwa na Ivan Rakitic dakika ya 82 kukamilisha ushindi huo ambao unaipa barcelona tiketi ya kucheza fainali ya kombe hilo dhidi ya Sevilla.
No comments