CONTE: BARCELONA NA MESSI WANANINYIMA USINGIZI
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte amesema anakosa usingizi akifikiria mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona na uwepo wa Lionel Messi.
The Blues wataikaribisha Barcelona usiku wa leo kwenye uwanja wa Stamford Bridge katika hatua ya mtoano ya michuano hiyo.
Licha ya ushindi wa ligi dhidi West Brom na kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la FA Cup bado Chelsea haipewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.
Matokeo ya mchezo huo huenda yakaamua mustakabali wa Conte ndani ya matajiri hao wa London kutokana na kutofautiana na mabosi wake.
"Siku hizi chache baada ya mchezo FA, kwakweli niwe muwazi ilikuwa ngumu kwangu kupata usingizi nikifikiria mchezo huu.
"Ukitaka kucheza mechi kama hii lazima ujiandae tena vizuri, kuandaa vitu vikubwa na maelekezo madogo tu," alisema Conte.

No comments