AJIBU NI 50/50 KESHO DHIDI YA ST LOUIS

Licha ya kurejea mazoezini mshambuliji nyota wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu hana uhakika wa asilimia mia wa kucheza mechi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi St. Louis.

Yanga itacheza na timu hiyo kutoka Shelisheli kesho jioni kwenye uwanja wa Taifa katika mchezo ambao wanahitaji matokeo ya ushindi kwa idadi nzuri ya mabao.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa 'Fuso' amesema mshambuliji huyo ameanza mazoezi jana pamoja na wenzake baada ya kupona maumivu ya miguu lakini hana uhakika kama atacheza kesho.

Nsajigwa amesema nyota huyo amerejea kikosini lakini bado hayupo fiti asilimia mia hivyo katika mchezo wa kesho itategemea na jinsi atakavyoamka.

"Ajibu amefanya mazoezi jana na leo lakini hayuko fiti asilimia mia kwahiyo anaweza kucheza mechi ya kesho au la," alisema Nsajigwa.

Kocha huyo amesema wachezaji Thaban Kamusoko, Pato Ngonyani, Juma Abdul, Youthe Rostand wamerejea kikosini na wamefanya mazoezi na wenzao baada ya kupona majeraha yao ingawa nao hawana uhakika wa kucheza kesho.

Wakati huo huo Amiss Tambwe, Donald Ngoma, Yohana Nkomola na Abdallah Shaibu hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho kutokana na kuwa majeruhi.

No comments

Powered by Blogger.