WAPENDASOKA WAANZA MWAKA KWA KUGAWA ZAWADI KWA WATOTO WENYE UHITAJI BAGAMOYO

Taasisi ya Wapendasoka Tanzania inayoundwa Na muunganiko wa vijana wa Tanzania wenye mapenzi Na mchezo wa Mpira wa miguu hapa nchini imeadhimisha sikukuu yao ya Wapendasoka Day ambayo huambatana Na sherehe za mwaka mpya Kila mwaka.

Wakiwawakilisha wenzao, vijana zaidi ya 30 Leo January 1, 2018 walifika Bagamoyo katika kituo cha kulelea watoto wenye uhitaji cha IMUMA ambapo pamoja Na kukabidhi zawadi mbalimbali, Wapendasoka walikula chakula cha mchana Na watoto hao.
C.E.O WA WAPENDASOKA ALIESIMAMA

Akizungumza katika hafla hiyo fupi, CEO wa Wapendasoka alisema waliamua kurejea katika kituo hicho cha IMUMA baada ya kujiridhisha kwamba uongozi wake upo makini Na watoto wana uhitaji.

Akizungumza baada ya kupokea misaada mbalimbali kutoka kwa Wapendasoka, mama mlezi wa kituo hicho Bi Asha Said Rashid amesema anawashukuru sana kwa moyo wao wa kujitolea na kukikumbuka kituo hicho mara kwa mara.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Wapendasoka Day 2018 Ndugu Al-Amin Lwano amesema anawashukuru sana wadau wote walioshiriki kwa namna yoyote kufanikisha shughuli hiyo kwa michango yao ya hali Na Mali.

Mapema mwanzoni mwa shughuli hiyo, Katibu Mkuu wa Wapendasoka Richard Leonce aliwaomba washiriki kuwa kimya kwa dakika Moja ili kumuenzi marehemu Shose Fidelis Masao ambaye mara ya Mwisho Wapendasoka walipoenda IMUMA alikua mmoja wao. Shose alifariki dunia kwa ajali ya gari Mei 28 mwaka 2017.

Sherehe nyingine za Wapendasoka Day zitafanyika tena January 1, 2019.


Powered by Blogger.