USHINDI WAIFANYA YANGA KUVUNJA REKODI CHAMAZI

Timu ya Yanga imekuwa ya kwanza kushinda mchezo wa ligi katika uwanja wa Azam Complex baada ya kuifunga Azam FC mabao 2-1.

Azam haikuwahi kupoteza mchezo wa ligi katika uwanja huo kabla ya kukutana na kipigo hicho kutoka kwa mabingwa hao.

Yanga haikupewa nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo baada ya wachezaji wake saba kuwa majeruhi huku Azam ikiwa kwenye kiwango bora.

Yanga imepanda hadi nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 28 ikizidiwa pointi nne na vinara Simba.

Kwenye mchezo huo mabao ya Yanga yalifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 30 na Gadiel Michael dakika 44 huku bao la Azam likifungwa Shaban Chilunda.


Matokeo ya mechi nyingine za ligi

Mwadui 2-2 Njombe Mji
Mbeya City 0-0 Mtibwa Sugar
Kagera Sugar 0-0 Lipuli FC

No comments

Powered by Blogger.