MFARANSA WA SIMBA AREJESHA 4G, OKWI NA BOCCO BALAA.
Kocha mkuu wa Simba Pierre Lenchantre ameanza na Ushindi wa 4-0 dhidi ya Maji maji ya Songea Leo katika mchezo wake wa kwanza tangu aanze kuwanoa Wekundu wa Msimbazi Simba akiziba nafasi ya Joseph Omog aliyetimuliwa na timu kubaki na kocha msaidizi tu.
Mchezo huo wa ligi kuu ya Soka Tanzania bara ulichezwa jioni hii katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam na mpaka Mapumziko Simba ilishakua mbele Kwa bao 2-0 magoli yote yakifungwa na Nahodha John Raphael Bocco.
Kipindi cha Pili Maji Maji walishindwa kabisa kuizuia safu ya ushambuliaji ya Simba iliyokua chini ya John Bocco na Mkongwe Emmanuel Okwi hivyo kuruhusu nyavu zao kutikiswa tena Mara mbili kama ilivyokua kipindi cha kwanza lakini safari hii mabao yote mawili yakifungwa na Emmanuel Okwi.
Tangu kukamilika Kwa michuano ya kombe la Mapinduzi kule Zanzibar Simba imeendelea kuonekana inaimarika Ikiwa imeshafunga mabao 10 KATIKA mechi tatu tangu kukamilika Kwa michuano Ile huku Ikiwa haijafungwa bao lolote mpaka sasa.
Ilianza Kwa kuifunga Singida United bao 4-0 kisha kuifunga Kagera Sugar bao 2-0 na Leo kuifunga Maji Maji bao 4-0 na ushindi wa Leo unaifanya Simba kufikisha pointi 35 katika nafasi ya kwanza Ikiwa ni pointi 5 mbele ya Azam FC wanaokamata nafasi ya pili na pointi 7 mbele ya Yanga wanaoshika nafasi ya tatu.

No comments