BEKI WEST HAM AFUNGIWA MECHI SITA KWA KUMTEMEA MATE MWENZAKE

Mlinzi wa West Ham United, Arthur Masuaku amefungiwa mechi sita na chama cha soka nchini Uingereza FA baada ya kumtemea mate mchezaji mwenzake.

Raia huyo wa Ufaransa alimtemea mate Nick Powell wa Wigan katika mchezo wa FA waliopoteza lakini hata hivyo beki huyo mwenye miaka 24 tayari ameomba radhi kwenye mitandao ya kijamii akisema sio tabia yake.

Masuaku hatocheza mpaka West Ham itakapo ikaribisha Manchester United katika uwanja wa London Machi 18.

Meneja wa Hammers, David Moyes ambaye anakosa idadi kubwa ya wachezaji kutokana na kuwa majeruhi amesema Masaku alifanya ujinga.

 "Masuaku anastahili adhabu yoyote itakayo tolewa nasi pia tutapata tunachostahili," alisema Moyes.

Masuaku atakosa mechi dhidi ya  Crystal Palace, Brighton, Watford, Liverpool, Swansea na Burnley.

No comments

Powered by Blogger.