YANGA NA SIMBA KUANZA NA VIBONDE CAF
Droo ya kupanga ratiba
ya michuano ya kimataifa ya vilabu barani Afrika imefanyika leo mchana kwa timu
za Tanzania kupangiwa wapinzani wao katika michuano hiyo
Yanga ataanza
kuchuana na St Louis ya Shelisheli, Yanga wakishinda mchezo huo watakutana na Mshindi wa mchezo kati ya Township Rolers ya Botswana au Merrikh ya Sudan.

Simba wao wataanza na Gendarmerie ya
Djibouti na wakifanikiwa kushinda mchezo huo watakutana na Green Buffaloes ya Zambia au El Masry ya Misri
Wawakilishi kutoka Zanzibar timu ya JKU imepangiwa Zesco
United ya Zambia ambayo nayo itaanzia nyumbani.
Zimamoto ambayo itashiriki michuano ya Shirikisho Afrika
kutokea Zanzibar imepangiwa timu ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia.
Mechi za awali zifanyika Februari 9-11 na marudio yatakuwa
Februari 16-18.
No comments