TANZANIA YAZIDI KUPOROMOKA VIWANGO VYA FIFA DUNIANI
Tanzania imezidi kuporomoka katika viwango vya ubora wa soka duniani baada ya kudondoka kwa nafasi tano zaidi kwa mwezi Novemba katika viwango vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la soka Ulimwengu ‘FIFA’.
Katika mwezi Oktoba Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya 142 kwa kuwa na alama 192 lakini katika viwango vya ubora vilivyotolewa Disemba 21, inaonesha Tanzania sasa inashika nafasi ya 147 kwa kukusanya alama 182.
Licha ya sare ya bao 1-1 Tanzania waliyoipata dhidi ya dhidi ya Benin kwenye mchezo wa kimataifa unaotambulika na FIFA uliofanyika Novemba 12 mjini Cotonou, lakini haijazuia kushika nafasi hiyo.
Hii ni Habari Mbaya kwa uongozi mpya wa soka nchini 'TFF' chini ya Rais Wallace Karia, kwani toka walipoingia madarakani Agosti 12 mwaka huu, Tanzania imekuwa ikiporomoka bila kupanda kwa nafasi yoyote.
Mwezi Julai ilikuwa nafasi ya 120, mwezi Agosti ikawa nafasi ya 125, mwezi Septemba ikaporomoka nafasi 11 na kushika nafasi ya 136, na mwezi Oktoba ikashuka tena hadi nafasi ya 142 na sasa inashika nafasi ya 146.

No comments