MTIFUANO EPL LEO NI ARSENAL VS LIVERPOOL EMIRATES
Mechi moja tu ya ligi kuu ya england Inatarajiwa kuchezwa leo katika dimba la Emirates nyumbani kwa timu ya Arsenal kuwania nafasi ya kuwa moja ya timu nne za juu katika msimamo wa ligi kuu ya England
Mechi baina ya miamba hiyo ni ufunguzi wa mzunguko wa pili wa ligi hiyo kukiwa na kumbukumbu mbovu kwa upande wa Arsenal baada ya kufungwa bao 4-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza pale Anfield
Liverpool inashika nafasi ya Nne ikiwa na pointi 34 wakati Arsenal wana pointi 33 katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Manchester City ambao hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa.
Silaha kubwa waliyonayo Liverpool ni safu kali ya ushambuliaji inayoongozwa na Mohammed Salah ambaye ni kinara wa kupachika mabao lakini wana safu mbovu ya Ulinzi ambayo mara nyingi imekua ikiruhusu kufungwa
Arsenal wao hawa tabiriki lakini siku za hivi karibuni wamekua wakicheza soka safi la kushambuli hivyo kufanya mechi ya leo kuwa ngumu kuifikiria
No comments