MOROCCO: UBINGWA NI LAZIMA KWA ZANZIBAR HEROES
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Hemed Morocco amesema anaamini kuwa mashabiki wa soka pamoja na Timu ya Kenya wataendelea kuishangaa pale watakapotwaa ubingwa wa Cecafa Challenji 2017
Kocha huyo ambaye amepata sifa kubwa nchini Kenya toka timu yake ilipoifunga Uganda kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Nusu fainali Ijumaa ya Disemba 15, amesema anajua fika kuwa Kenya ni timu nguvu lakini hawatazembea hadi wahakikishe wanatwaa ubingwa huo.
Hemed amesema kiburi hicho kinakuja wakati ambapo Zanzibar imekaa muda mrefu tangu watinge hatua ya fainali, na mara ya mwisho walipofikia hatua hiyo walitwaa ubingwa kwa kuwafunga Uganda tena katika ardhi yao.
-Ni kitu kizuri kufika fainali ukilinganisha na timu zote ambazo zilikuwa kwenye mashindano, hii ni faraja kubwa kwetu sisi, hatujachukua kombe hili muda mrefu pamoja na kuwa kufikia hatua hii tunaimani kubwa tutachukua kombe hili, amesema.
No comments