LIPULI YAMUANDIKIA BARUA KWASI KUMTAHADHARISHA

Klabu ya Lipuli FC 'Wanapaluhengo' yenye maskani yake mkoani Iringa imesema imemuandikia barua mchezaji wake Mghana Asante Kwasi kuripoti mapema kazini Kabla hatua za kinidhamu hazijachukuliwa dhidi yake.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Ramadhan Mahano amesema Kwasi alitakiwa kuwa awe ameripoti tangu Disemba 17 lakini mpaka sasa bado hajaripoti kazini jambo ambalo wamelitafsiri ni utovu wa nidhamu.

Tumemuandika barua (Kwasi) kumtahadhalisha kuhusu kitendo chake cha kutofika kazini, alitakiwa awe amefika kambini toka Jumapili lakini hadi sasa hivi hatujamuona, ajue tu kuwa bado ni mchezaji wetu na anatakiwa kuheshimu taratibu za klabu," Mahano amesema.

No comments

Powered by Blogger.