KOCHA WA SIMBA AWAAHIDI MAMBO MAZURI MASHABIKI
Kocha aliyekabidhiwa majukumu mazito ya kukinoa kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club, Masoud Djuma amesema mipango yake baada ya kupewa kikosi hicho ni kurudisha heshima na morali.
Amesema atafanya hivyo kwa wachezaji mashabiki na wanachama wa timu hiyo ambao kwa kuanzia ni lazima aifunge Ndanda FC kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa mjini Mtwara.
Mashabiki na wanachama wamepoteza imani na timu yao, lakini nitahakikisha imani yao inarejea na hiyo ni kushinda mechi zijazo. Bado timu ni nzuri na kikosi ni kipana,” amesema.
Djuma alisema katika mazoezi ya Jumapili asubuhi alitumia muda wake kuzungumza na wachezaji ili kila mmoja kujua jukumu lake ndani ya timu, Nataka kila mchezaji aelewe jukumu lake uwanjani, kwani tunachohitaji sasa ni ushindi pekee na si kitu kingine, hivyo Wana Simba wategemee baadhi ya mabadiliko yenye mafanikio katika timu yao,” aliongeza.
Djuma alisema mipango yake ni kurejesha Simba katika kiwango bora kwani anafahamu kiu ya Wanasimba wote ni mafanikio na kutwaa ubingwa wa ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

No comments