KENYA WATWAA UBINGWA WA CECAFA

Timu ya Taifa ya Soka ya Kenya wametawazwa mabingwa wa michuano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati 'CECAFA' kwa kuifunga Zanzibar jumla ya penati 3-2 baada ya dakika 120 kumalizika kwa Sare ya 2-2.

Mpaka mapumziko Kenya walikuwa mbele kwa bao moja kwa bila, Kipindi cha pili Zanzibar Heroes walikuja wakiwa na ari zaidi wakitafuta bao la kusawazisha na pengine kupata bao la ushindi.


Khamis Mussa aliisawazishia Zanzibar dakika ya 87 baada ya kumalizia mpira wa krosi na mlinzi wa kushoto Hajji Mwinyi.

Wenyeji walipata bao la pili dakika ya 97 kupitia kwa Choka Masoud kabla ya Khamis kusawazisha tena dakika mbili baadae.

Wachezaji wa Zanzibar Heroes waliokosa penati ni Adeyun Saleh, Issa Dau, Mohammed Issa 'Banka' wakati Feisal na Mudathir wakifunga.

Penati za Kenya zilifungwa na Atudo Otieno, Onguso Arasa na Ouma Onyango wakati Otieno Duncan akikosa penati yake.

No comments

Powered by Blogger.