TFF KUTOA MAFUNZO SOKA LA UFUKWENI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litatoa mafunzo ya soka la ufukweni (Beach
Soccer) kwa vyuo mbalimbali hapa nchini vilivyothibitisha kushiriki Ligi
Maalumu ya soka la Ufukweni itakayoanza Novemba 18, 2017.
Kwa upande wa mafunzo
ni kwamba yatafanyia siku tano kabla ya kuanza kwa ligi hiyo ambako itakuwa ni
Novemba 13, mwaka hu. TFF imepanga kutoa mafunzo hayo kwa vyuo hivyo ili
wauelewe zaidi mchezo huo pamoja na sheria zake.
Tumepeleka mchezo huo
kwenye vyuo ili kutoa hamasa ya soka la ufukweni kuenea zaidi na kuweka hazina
ya wachezaji wa timu ya taifa.
Mpaka sasa vyuo 14
tayari vimethibitisha kimaandishi kushiriki kwenye mafunzo hayo.
Vyuo vilivyothibitisha
kushiriki ni Chuo cha Ardhi, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo Cha Ufundi
(DIT), Chuo cha Usafirishaji (NIT), Chuo cha Elimu ya Tiba cha Kahiruki, Chuo
cha Elimu ya Biashara cha Lisbon, Chuo cha Silva , Chuo UAUT, TIA, El-Maktoum
collage Engineering, Magogoni, Chuo cha uandishi wa habari DSJ na TSJ.
Mafunzo hayo
yatatanguliwa na tukio la kukutana na viongozi wa vyuo shiriki hapo Novemba 10,
2017.
Wakati huo huo kozi ya
waamuzi wa Soka la Soka la Ufukweni imeanza leo Novemba 7, 2017 katika Makao
Makuu ya TFF Karume, Dar es Salaam ambayo yanatarajiwa kumalizika Novemba 12,
2017.
No comments