CHELSEA YAPIGWA 'TATU MZUKA' LIGI YA MABINGWA ULAYA, ATLETICO MADRID YABANWA NYUMBANI
Mzunguko wa pili wa hatua ya makundi katika ligi ya mabingwa barani Ulaya umeanza usiku wa jumanne na utamalizika usiku wa \jumatano katika viwanja mbali mbali barani humo.
Jijini Roma Italia mechi moja ya kundi C ilishuhudia wenyeji AS Roma waliwaalika mabingwa wa England Chelsea na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 3-0 mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Olimpiki jijini Roma.
Stephan El Sharaawy alitangulia kuipatia Roma bao la kuongoza dakika ya kwanza tu ya mchezo kisha kuongeza bao la pili dakika ya 36 kabla ya Diego Perotti hajafunga bao la tatu na la mwisho kwa Roma ambao wamemkaribisha nchini Italia Antonio Conte kocha wa Chelsea.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo C wenyeji Atletico Madrid wakiwa nyumbani walikubali sare ya bao 1-1 huku timu zote zikimaliza zikiwa pungufu baada ya wachezaji wawili kutolewa kwa kadi nyekundu.
Matokeo hayo yanaifanya Roma kufikisha pointi 8 ikiwa ndiyo kinara wa kundi hilo wakati Chelsea wana point 7 na atletico Madrid wakiwa na pointi 4
No comments