ALAN PARDEW NDIYE KOCHA MPYA WA WEST BROMWICH ALBION

West Bromwich Albion have confirmed former Newcastle boss Alan Pardew as their manager
Klabu ya Ligi kuu ya England West Bromwich Albion imemtangaza aliyekua kocha mkuu wa Chalton, Newcastle United na Crystal Palace Alan Pardew kuwa mkufunzi wake mkuu.

Taarifa ya uteuzi wa kocha huyo imetoka leo ikiwa ni masaa kadhaa tangu West Brom walipolazimishwa sare ya bao 2-2 dhidi ya Newcastle United wakiwa tayari walishakua wanaongoza kwa bao 2-0.

Pardew alikua nje ya soka kwa muda kadhaa baada ya kutimuliwa kazi msimu uliopita akiwa na Crystal Palace na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Tony Pullis aliyetimuliwa mapema mwezi huu baada ya mfululizo wa matokeo mabaya.

West Brom wanakamata nafasi ya 16 hivi sasa wakiwa na pointi 12 baada ya michezo 14 ukiwa ni msimu wao wa tano mfululizo kwenye ligi kuu ya England bila kuteremka daraja 

No comments

Powered by Blogger.