YANGA YABANWA NA KMC YA MINZIRO
Ikiwatumia wachezaji wengi wa timu ya akiba timu ya Yanga imelazimishwa sare ya bila kufungana na KMC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex usiku huu.
Yanga ilitangaza wiki iliyopita kuwa mapato yatakayopatikana kupitia mchezo huo yataingizwa katika ukarabati wa uwanja wa Kaunda ili kuanza kuutumia kwa mazoezi kuanzia msimu ujao.
Nyota kama Kabamba Tshishimbi, Gofrey Mwashiuya, Emmanuel Martin na Vincent Andrew ndio wachezaji wanaopata nafasi kwenye kikosi cha kocha George Lwandamina ambao walianza kwenye mchezo huo.
Kiungo chipukizi Maka Edward alionyesha kiwango safi kwenye mchezo huo huku mlinda mlango Beno Kakolanya nae akidaka kwa mara ya kwanza tangu arejee kutoka majeruhi.
Kwa upande wa kocha wa KMC, Fred Minziro ambaye kikosi chake kinaongoza kundi A la ligi daraja la kwanza alitumia pia wachezaji wengi ambao hawapi nafasi kubwa ya kucheza.

No comments