UWANJA UMECHANGIA MASHABIKI KIDUCHU 'KARIAKOO DERBY'


Uongozi wa klabu ya Simba umesema moja ya sababu iliyochangia kuwa na idadi ndogo ya mashabiki walijitokeza kwenye mchezo wa watani Jumamosi iliyopita ni uwanja wa Uhuru.

Uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 23,000 ulitumika kwenye mchezo huo baada ya ule wa taifa kuwa katika ukarabati mkubwa.

Msemaji wa Wekundu hao Hajji Manara amesema kuwa mashabiki waliohofia usalama wao kutokana na udogo wa uwanja huo huku mchezo wenyewe ukihusisha watu wengi.

"Simba na Yanga ndio klabu kubwa nchini hilo halina ubishi, kupanga mchezo kwenye uwanja wa Uhuru kumesababisha idadi ndogo ya mashabiki.

"Tangu nimeanza kuangalia mechi ya Simba na Yanga sijawahi kushuhudia idadi ndogo ya mashabiki kama ile, watu waliogopa kuja uwanjani kutokana na uwanja kuwa mdogo hivyo kuhofia usalama wao," alisema Manara.

Msemaji huyo ameitaka bodi ya ligi kufikiria mara mbili linapokuja suala la Simba na Yanga katika michezo ijayo.

1 comment:

  1. Sasa ndo nini kaongea Manara
    mi nilijua ameita waandishi kuongea jambo la maana wala swala sio udogo wa uwanja kiingilio cha elfu 10 kilipunguza sana idadi ya watu mbona Simba na Azam japo uwanja ni mdogo lakini ulijaa kwani swala la usalama halikuwepo?

    ReplyDelete

Powered by Blogger.