UFARANSA NA URENO ZATINGA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA, UHOLANZI NJE

The home side celebrate their automatic qualification for next year's World Cup with supporters following the final whistle
Mabingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Ureno pamoja na Ufaransa jana ziliungana na matifa mengine makubwa Duniani ambayo tayari yameshafuzu kwa fainali zijazo za kombe la Dunia zitakazopigwa nchini Russia.

Ureno ikiwa nyumbani iliibuka na ushindi wa bo 2-0 dhidi ya Uswisi  katika dimba la Estadio da Luz magoli yakifungwa na Andre Silva na goli la kujifunga la beki wa zamani wa Arsenal Johan Djourou na kuifanya Ureno kufikisha pointi 27 katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi B huku Uswis wao wakipata nafasi ya kucheza mechi za mtoano baada ya kumaliza kundi wakiwa na pointi 27 pia katika nafasi ya pili.

Ufaransa ikicheza nyumbani iliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Belarus mabao ya mshmabuliaji wa Arsenal Olivier Giroud na Antoine Griezman matokeo yanayoiweka Ufaransa kileleni mwa kundi A wakiwa na pointi 23 huku Sweden ikishika nafasi ya pili licha ya kufungwa bao 2-0 na Uholanzi na kufanya timu zote hizo kumaliza wakiwa na pointi 19 huku Sweden ikiwa na faida ya magoli


No comments

Powered by Blogger.