TAIFA STARS KAMILI KUIVAA MALAWI LEO

Timu ya Soka ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars leo inacheza mchezo wa kirafiki dhidi Malawi jijini Dar es salaam katika Uwanja wa Uhuru.

Kiingilio katika mchezo huo wa kirafiki ni elfu  3,000 mzunguko na jukwaa kuu 5,000

Kocha wa Taifa Stars Salum Mayanga amesema Vijana wake wapo tayari kutokana na maandalizi mazuri waliyofanya kwa wiki nzima na kikosi chake.


Amewaomba watanzania waje kwa wingi kuisapoti timu hiyo ambayo inajiandaa na mechi za kufuzu Afcon 2019.

No comments

Powered by Blogger.