STARS PUNGUFU YABANWA MBAVU NA MALAWI UHURU
Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imebanwa mbavu kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Malawi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Kocha wa Stars, Salum Mayanga ameendelea kuwa na rekodi nzuri katika timu hiyo baada ya kuiongoza katika michezo 13 akifungwa mechi moja pekee.
Katika mchezo huo Stars ilimaliza ikiwa na wachezaji tisa uwanjani kufuatia Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na mchezo usiokuwa wa kiungwana.
Wenyeji walikuwa bora zaidi kipindi cha kwanza kwa kumiliki sehemu kubwa ya mchezo iliyopelekea kupata bao dakika ya 35 lililofungwa kwa kichwa na Ngambi Robert.
Stars walisawazisha bao hilo dakika ya 57 kupitia kwa winga Simon Msuva kwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja wavuni.
Kiungo Hamis Abdallah anayechezea timu ya Sony Sugar ya Kenya alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kutolewa dakika ya 11 kufuatia kupata maumivu mguuni.

No comments