SIMBA YAICHAPA DODOMA FC YA JULIO NYUMBANI KWAO

Bao pekee la dakika ya 69 lililofungwa na kiungo Said Ndemla limetosha kuipa Simba ushindi dhidi ya Dodoma FC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Ndemla alifunga bao hilo kwa shuti kali mbele kidogo ya duara la kati ya uwanja lililomshinda mlinda mlango Jackson Chove.

Dodoma inayonolewa na kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' ilionyesha ukakamavu mbele ya Simba na kuwabana Wekundu hao hali inayo onyesha wanaweza kupanda daraja kushiriki ligi kuu msimu ujao.

Timu hiyo inashiriki ligi daraja la kwanza inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi sita baada ya mechi tatu ikishinda mechi mbili na kupoteza moja.

Kocha wa Simba Joseph Omog aliwatumia wachezaji ambao hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza huku nahodha wazamani wa Wekundu hao Jonas Mkude aking'ara katika eneo la kiungo.

No comments

Powered by Blogger.