NGOMA,TAMBWE,KAMUSOKO NDANI JUMAMOSI DHIDI YA MNYAMA
Benchi la ufundi la timu ya Yanga limepata uhueni
baada ya wachezaji wake watatu Amiss Tambwe,Donald Ngoma na Thaban Kamusoko
kujiunga na wenzao kambini baada ya kupona majeruhi
Kikosi cha Yanga kipo kambini mkoani Morogoro kwa
ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Simba utakaofanyika
kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Jumamosi ijayo.
Nyota hao raia wa kigeni walikuwa majeruhi kwa muda
wakikosa baadhi ya mechi huku Tambwe akiwa hajapata nafasi ya kucheza mechi
hata moja mpaka sasa.
Msemaji wa klabu hiyo Dismas Ten amesema wachezaji
hao wamejiunga na wenzao kambini mkoani Morogoro leo tayari kwa mchezo huo.
"Wachezaji wetu Ngoma, Tambwe na Kamusoko
wamejiunga kambini leo na wenzao mwalimu atakapoona inafaa kuwatumia kutokana
na kupona majeraha," alisema Ten.
Timu zote zina pointi 15 huku Simba ikiongoza kwa
idadi ya mabao ya kufunga.

 
 
 
No comments