NCHI TATU ZAGOMBEA UENYEJI CHAN
Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) limethibitisha kupokea maombi ya
nchi tatu ambazo ni Equitorial Guinea, Ethiopia na Morocco wametuma maombi ya
kuandaa mechi za taifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za
ndani (CHAN).
Morocco ilithibitisha
ombi lao siku ya Jumamosi, nao Caf wakatangaza jana Jumapili kuwa pia kulikuwa
na maombi kutoka nchini Ethiopia na pia Equitorial Guinea, ambao waliandaa
mechi za taifa bingwa barani Afrika mwaka 2015.
Caf wanatafuta
mwenyeji mpya kuchukua nafasi ya Kenya ambayo ilipoteza fursa hiyo baada ya
kushindwa kutimiza matakwa ya shirikisho la Caf
No comments