"MAAJABU YA MESSI" YAIPELEKA ARGENTINA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA MWAKANI
Lionel Messi pengine ni jina linalotajwa zaidi sasa na pengine kwa siku nzima hii ya leo na Mamilioni ya Wapenda Soka Duniani kutokana na Ushujaa wake aliouonyesha kwa taifa lake la Argentina wakati ambapo mashaka yalishaingia kwamba pengine Argentina ingekosa nafasi ya kushiriki kwa Kombe la Dunia mwakani kule Russia.
Messi alifunga mabao yote matatu katika ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Wenyeji Ecuador katika mechi ya mwisho ya kusaka nafasi ya kucheza katika fainali za kombe la Dunia mwakani fainali ambazo zitachezwa katika nchi ya Russia.
Hii ilikua mechi ya kushinda ili kuweza kupata nafasi ya moja kwa moja kushiriki fainali hizo huku matokeo ya nyuma yakifanya wengi wakiwa na mshaka kwamba Argentina huenda ingeshindwa kupata moja kati ya nafasi nne za moja kwa moja huku Ecuador wakitangulia kufunga bao la uongozi dakika ya kwanza tu ya mchezo kupitia kwa Romario Ibarra lakini Messi yeye akafunga bao la kusawazisha dakika ya 11 kisha akaongeza la pili dakika ya 18 na kumalizia la tatu dakika ya 62.
Matokeo hayo yanaifanya Argentina sasa kufikisha pointi 28 katika nafasi ya 3 ukanda wa Amerika ya Kusini ikiungana na Brazili wenye pointi 41, Uruguay pointi 31 na Colombia pointi 27 huku Peru yenye pointi 26 ikipata nafasi ya kucheza mechi ya mtoani dhidi ya New Zealand.
No comments