YANGA KUMKOSA TSHISHIMBI DHIDI YA MTIBWA SUGAR


Kiungo wa Yanga Kabamba Tshishimbi alioneshwa kadi ya njano katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Ndanda FC uliochezwa Jumamosi ya September 13 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kadi hiyo ilikua ni ya tatu kwake pamoja na zile alizooneshwa katika michezo iliyopita, hali inayompelekea nyota huyo sasa kuadhibiwa kwa kukosa mchezo mmoja unaofuata ambao kwa mujibu wa ratiba, Yanga watakutana na Mtibwa Sugar Jumamosi katika uwanja wa Uhuru.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tshishimbi amewaomba radhi mashabiki wa soka huku akisema kwamba makosa aliyoyafanya aliyafanya kwa ajili ya klabu yake.

"Samahani, nitakosa mchezo ujao kutokana na kadi tatu za njano lakini nitarejea baada ya mchezo huo ambapo Yanga Itasafiri kuwavaa kagera Sugar. Yote niliyafanya kwa ajili ya klabu. Ilisema taarifa hiyo fupi.

Tshishimbi amekua akitumika kama kiungo mkabaji katika michezo yote ya Yanga msimu huu. Hata hiyo Yanga watalazimika kuziba pengo lake kwa kumtumia Said Juma au Pato Ngonyani.

No comments

Powered by Blogger.