SIMBA YASEMA OMOG HAENDI POPOTE
Uongozi wa timu ya soka ya Simba SC umemaliza uzushi
uliokuwa ukiendelea kuwa klabu hiyo imetoa mechi 5 kwa kocha Joseph Omog ili
iweze kumtimua kazi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo Said Tully alisema maneno hayo ya
kumpa michezo mitano kocha huyo wa Cameroon ni uongo na hawajui nani kaanzisha.
‘’Ni uzushi mtupu hutatamtimua kocha wetu Joseph
Omog,Habari rasmi lazima itokee kwa klabu yetu tunaomba wadau,wapenzi pamoja na
wanachama wasisikilize maneno haya bali wayapuuze’’Tully alisema.
Akielezea kuhusu matokeo ya timu yao,Tully alisema
mpaka sasa timu yao haijafanya vibaya katika ligi kwa kuwa imecheza michezo
minne na imeshinda miwili dhidi ya Ruvu shooting na Mwadui. Huku ikiwa imetoka
sare ugenini dhidi ya Mbao FC na Azam FC.
Tully alisema walimu wao wote wawili Jackson
Mayanja na Joseph Omog wanafanya kazi nzuri sana na Uongozi wao una imani kuwa
watafanya vyema katika msimu huu wa ligi kuu.
Kwa upande wake msemaji wa timu ya soka ya Simba SC
Haji Manara alisema timu yao ina imani kubwa sana na kocha Omog kwa mafanikio
aliyowapa.
Manara alisema watu wasiopenda klabu yao wamekuwa
wakizusha uvumi kuwa timu yao itamfukuza kocha huyo jambo ambalo si jema.
No comments