MAYANGA ATANGAZA KIKOSI KITAKACHOIVA MALAWI

Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga ametangaza kikosi kipya kitakachocheza na Malawi ‘The Flame’ katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Oktoba 2 hadi Jumatano ya Oktoba 11, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Malawi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Oktoba 7, 2017 katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni.

Katika kikosi hicho cha wachezaji 22, Kocha Mayanga ambaye aliteuliwa Januari 4, mwaka huu ameita nyota watano wanacheza soka nje ya mipaka ya Tanzania akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.

Kikosi hicho kinachotarajiwa kuingia kambini Ijumaa Oktoba mosi, mwaka huu kwenye Hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam

Makipa;
Aishi Manula (Simba), Peter Manyika (Singida United) na Ramadhani Kabwili (Yanga SC).

Mabeki;
 Gardiel Michael (Yanga), Boniface Mganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Kelvin Yondan (Yanga), Salim Mbonde (Simba)Adeyuni Salehe (Stand United) na Erasto Nyoni (Simba).

Viungo;
 Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdalla (Sony Sugar, Kenya), Muzamil Yassin (Simba), Simon Msuva (Difaa Hassan El- Jadida, Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (Tenerrife B, Hispani) Ibrahim Ajib (Yanga Sc) Abdul Hilal Hassan na Morel Ergenes (Ureno).

Washambuliaji;
Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji) na Mbaraka Yusuph (Azam FC).

No comments

Powered by Blogger.