AZAM NI MWENDO WA USHINDI KIMYA KIMYA KIMYA LIGI KUU TANZANIA BARA


Wana Lambalamba Azam FC wameendelea kufanya vyema katika mechi zao za ligi kuu Tanzania bara msimu huu na hapo jana waliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Mshambuliaji aliyesajiliwa na Azam FC toka Kagera Sugar Mbaraka Yusuph ndiye aliyewaliza waajiri zake hao wa zamani kwa kufunga bao lake dakika ya 43.

Matokeo hayo yanaifanya Azam Fc kufikisha pointi 7 baada ya mechi 3 msimu huu wakianza ligi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda kisha kutoka sare na Simba wiki iliyopita na jana kuwafunga Kagera sugar bao 1-0.


No comments

Powered by Blogger.