YANGA YAENDELEA KUTESTI MITAMBO YAICHAPA SINGIDA UNITED
Mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara leo wamecheza mchezo wao rasmi wa kwanza wa kujipima ubavu dhidi ya wageni wa ligi Singida United kutoka Singida katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliokua wa kusisimua kutokana na vikosi vyote kuwa katika hatua za mwisho za maandalizi ya msimu mpya, Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Pamoja na kufungwa leo, Singida United walionesha kandanda safi sana na la kuvutia, wakionekana kuonana vyema zaidi ya Yanga ambao miili yao haikuonekana kuwa katika hali nzuri, labda kutokana na mazoezi magumu.
Yanga walikua wa kwanza kupata bao katika kipindi cha kwanza likifungwa na kiungo Thabani Kamusoko kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja kimiani.
Haikuwachukua muda mrefu Singida United kusawazisha bao hilo kupitia Danny Usengimana ambaye alifunga kwa kichwa akiunganisha vyema krosi ya beki Michael Rusheshangoga ambaye alimzidi maarifa Haji Mwinyi.
Kasi na uwezo binafsi wa mshambuliaji Simbarashe Nhivi wa Singida United haikumuacha salama nahodha wa Yanga, Nadir Haroub, kwani alijikuta akipitwa kirahisi na Nhivi kuiandikia Singida bao la pili lililoipeleka timu yake mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili, Yanga walionekana kufanya mabadiliko mengi kwa ajili ya kuwajaribu wachezaji wao ambapo wachezaji kama Beno Kakolanya, Donald Ngoma, Ibrahim Ajibu, Haji Mwinyi, Juma Abdul, Calvin Yondani, Raphael Daudi na Baruan Akilimali walitoka na nafasi zao zikachukuliwa na Youthe Rostand, Emmanuel Martin, Juma Mahadhi, Andrew Vicent, Bonyang, Harry, Maka Mwakalukwa, Amisi Tambwe na Said Musa.
Yanga walisawazisha kwa penalt kupitia Amisi Tambwe dakika ya 86 baada ya golikipa wa Singida, Said Lubawa kumwangusha Said Musa katika eneo la hatari.
Ndani ya dakika tatu za nyongeza kabla ya mchezo kumalizika, shuti la mbali la Emmanuel Martin lilimshinda golikipa Said Lubawa na kutinga wavuni kuiandikia Yanga bao la tatu.
Hadi mwisho wa mchezo, Yanga 3-2 Singida.

No comments