SWANSEA YASHINDWA KUIZUIA KASI YA MAN UNITED,YAPIGWA VIBAYA NYUMBANI


Manchester United imeendelea kugawa dozi katika msimu mpya wa ligi kuu ya England wakishinda tena bao 4-0 ugenini.

Swansea City ndiyo waliokuwa wenyeji wa United leo na kujikuta wakishindwa kabisa kuzuia kasi ya Manchester United ambayo ilishinda pia bao kama hizo kwenye mechi iliyopita dhidi ya West Ham.

Eric Bailly alitangulia kuipatia United bao la kwanza dakika ya moja tu kabla ya mapumziko na kuifanya United kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao hilo moja.

Kipindi cha pili kilikua kigumu zaidi kwa Swansea ambao walikubali kufungwa mabao matatu zaidi kupitia kwa Romelu Lukaku,Paul Pogba na Antony Martial.

United imefikisha pointi 6 baada ya michezo miwili ikifunga pia magoli 8.

No comments

Powered by Blogger.