PENATI ZAIZAMISHA YANGA TAIFA NA KUIPA SIMBA USHINDI

Mabingwa wa kombe la Azam Sports Federation Cup, Simba ya Dar es Salaam leo wamefanikiwa kutwaa ngao ya jamii baada ya kuwafunga Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Yanga kwa penalt 4-5.


Mchezo huo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa sare ya kutofungana katika dakika ya 90.

Penati tano tano zilipigwa na timu zote mbili ambapo penati nne ziingia kimiani kwa timu zote ambapo penati za Yanga zilifungwa na Kabamba Tshishimbi, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Ibrahim Ajibu wakati penati ya Kelvin Yondani ikipanguliwa na golikipa wa Simba Aishi Manula.

Kwa upande wa Simba, penati zilifungwa na Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi, Method Mwanjale na Shiza Kichuya. Penati ya Mohamed Hussen ilipanguliwa na golikipa Youthe Rostand.

Baada ya penati tano tano, ilibidi zipigwe penati moja moja ambapo Juma Mahadhi wa Yanga alipaisha penati yake kabla ya Mohamed Ibrahim kuifungia Simba na kuiwezesha kutwaa ngao ya jamii.

No comments

Powered by Blogger.